Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema Chama hicho kitazindua mikutano ya hadhara Januari 21, 2023 kwakuwa tarehe hiyo ni kumbukumbu ya siku waliyopewa usajili wa kudumu.
“January 21 ni siku kubwa yenye historia ndani ya Chama chetu, Chama chetu kilipata usajili wa kudumu January 21, 1993 kwahiyo tunapozindua mikutano ya hadhara tarehe hiyo, Chama chetu kinatimiza miaka 30 tangu kipate usajili huo na ndio maana tumechagua kwamba baada ya miaka saba ya kutofanya mikutano ya hadhara tuanze siku hiyo"
"Uzinduzi huo utaambana na uzinduzi wa ajenda za Kitaifa za mikutano ya hadhara, kesho Jumatatu tutaenda kulipia viwanja kwa sababu vingine vinamilikiwa na Halmashauri na tutapeleka taarifa Polisi kwa ajili ya kupatiwa ulinzi na hatutegemei kutakuwa na figisu."