Katika kitabu chaa Mhubiri 3:1-8, kila kitu humu duniani kina majira na wake. "Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake: Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa; wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; wakati wa kulia na wakati wa kucheka."
Huenda pia ni kutokana na mstari huo wa bibilia ndiyo sababu za kahaba mmoja kukata kuokoka akisema bado wakati na majira yake haijafika. Yote tisa video moja inasambaa kwenye mitandao ya jamii ikimuonyesha kahaba akimsuta mwinjilisti aliyejaribu kumhubiria wokovu.
Mrembo huyo ambaye alikuwa amesimama kwenye eneo lake la kuwavizia wateja, alikaribiwa na mwinjilisti huyo wa kike aliyedai kuwa aliongozwa na roho kumhubiria injili ya wokovu. Huku mtumishi huyo wa Mungu akijaribu kutoa sababu zake kumtaka kutubu na kuishi maisha ya wokovu, mrembo huyo alisikika akimkaripia na kusema: "Kuna wakati wa kila kitu, na ni wazi huu haukuwa wakati kwa sababu niko kazini."
Chanzo: TUKO.co.ke