Mwanaume mmoja raia wa Nigeria aliyetambulika kwa jina la Nkanu, amefunga pingu za maisha na wanawake wawili siku moja katika jimbo la Cross River.
Nkanu aliwaoa Mary na Jennet siku moja katika sherehe ya harusi iliyofanyika Jumamosi, Disemba 31, 2022, katika Uwanja wa Michezo wa Bazohure.
Picha za harusi hiyo ya kufana zilipakiwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwachangamsha wengi.