CCM yajitabiria ushindi wa kishindo 2025


Chama cha Mapinduzi (CCM), kimejitabiria kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.


Akizungumza katika hafla ya kufunga matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), visiwani Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdulla Juma Mabodi, amesema ushindi huo utatokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Hali inayoonekana 2025 mambo yatakwenda Bam Bam kwa jinsi unavyoendesha nchi hii, jinsi CCM iliyosimama imara na jinsi wana wa CCM wa ngazi zote wanavyosimamia utekelezaji wa ilani pamoja na dola unayoiongoza kwa ajili ya ushindi wa kishindo wa chama chetu,” amesema Mabodi.

Katika hatua nyingine, Mabodi amempongeza Rais Samia na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, kwa kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya CCM, kwa kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Rehema Sombi, amesema umoja huo uko tayari kupokea maelekezo ya viongozi wa juu wa chama hicho kwa ajili ya kuyatekeleza ili kipate ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

“Tupo tayari kupokea maelekezo kutoka chama na kuyafanyia kazi, lakini nishukuru kwa sense iliyofanyika 2022 imeonesha idadi kubwa ya watanzania ni vijana. Vijana hawa wataenda kuchukua na kuweka waaa 2025, pia sisi hatutasita kuendelea kuyasema yote mazuri yanayofanywa na Serikali yetu sikivu chini ya Dk. Samia,” amesema Rehema.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Khenani Kihongosi, amesema umoja huo utatumia mikutano ya hadhara iliyofunguliwa hivi karibuni kufanya siasa za kistaarabu pamoja na kuwaleeza wapinzani namna gani Serikali ya CCM inavyofanya kazi kubwa.

“Katika utwala bora tumeshuhuduia ukomavu wako wa kiuongozi kwa kufanya vikao vya maridhiano na vyama vya siasa nchini na kuridhia mikutano ya hadhara kwa vyama, tunashukuru Rais na sisi kama CCM tutakwenda kufanya siasa na kueleza wapinzani wetu namna gani Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa katika taifa hili,” amesema Kihongosi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo