CCM waibomoa CHADEMA Mufindi, Yakomba wanachama wake


Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kimempokea mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na wenzake zaidi ya 20 katika kata ya Mapanda.


Akizungumza wakati wa ziara kuimarisha chama, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke alisema kuwa wamempokea aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Mapanda na wenzake baada ya kuridhika kutokana na utendaji wa kazi wa viongozi wa chama cha mapinduzi.

Kavenuke alisema kuwa diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga amekuwa anafanya kazi nzuri ambayo imekuwa ikiwavutia watu wengi wakiwemo wapinzani ambao sasa wameamua kuungana na chama hicho.

Alisema kuwa ukiwa na viongozi wa kata kama diwani Obadia Kalenga ambao wanatekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi CCM inavyotakiwa inasaidia kukijenga chama kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa.

Kavenuke alimkaribisha Isaya Kitinusa katika chama cha mapinduzi kwa ajili ya kufanya nao kazi kwa kuwa chama cha mapinduzi ndio chama cha mfano katika Bara la Africa na duniani kwa namna ambavyo kinaendesha siasa zake.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mapanda Obadia Kalenga alisema kuwa amekuwa anafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wananchi wote wa kata ya hiyo ndio maana wapinzani wamekosa sehemu ya kukosoa ndio maana wamerudi katika chama cha mapinduzi.

Kalenga alisema kuwa sio mara kwanza wapinzani kutoka chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kujiunga na CCM katika kata hiyo hilo limekuwa linajitokeza kila wakati toka amechaguliwa kuwa Diwani wa kata ya Mapanda.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi CCM kama ambavyo inavyotaka ili kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo