Babu wa miaka 97 Aliyeoa binti Mchanga ajuta, aangua kilio


Babu wa miaka 97 ambaye alioa kigori wa umri wa miaka 30 sasa ameanza kulia kulemewa na mzigo wa binti huyo.


Mzee Batuuk anasema Alice Jepkorir ana watoto watano ambao wanafaa kupewa ulezi lakini hali yake haimruhusu.



Johanna Batuuk alifunga pingu za maisha kwa mara ya kwanza Januari 14,2023 kwa mpenzi wake Jepkorir ambaye ana watoto hao. Huku wanamtandao wakisema kuwa kigori huyo aliamua kuolewa kama mbinu ya kupata mali ya mzee huyo, Batuuk ameambia runinga ya NTV kuwa hana chochote maishani.


"Ni kweli nilifunga pingu za maisha lakini mimi sina chochote. Shamba langu limejaa mawe na nimeshindwa hata kulipia watoto karo na kuwalisha. Nisaidieni hata hii nyumba niweze kupata umeme," alisema Mzee Batuuk. Boma lao ni kweli linaonyesha umaskini huku nyumba ya matope ambayo haiwezi kustahimili vishindo ikiwakondolea macho wageni mithili ya mbwa aliyekonda kutokana na njaa. Batuuk alisema tofauti na tetesi za wengi kwamba kipusa huyo ananyemelea mali yake, yeye ndiye anapata usaidizi.


"Ni yeye ananisaidia kwa sababu mimi sina chochote," aliongeza mzee huyo wakati wa mahojiano kuhusu penzi lao. Alice alisema yeye anafuraha kukutana na ndume huyo na watoto wake tayari wanamtambua kama baba yao. Kisa cha wawili hao kimekuwa kikizua gumzo kali huku wengi wakisema ni kisa cha mzee kununua gazeti ambalo hataweza kulisoma. 

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo