Watu wawili wakazi wa mtaa wa Msakasaka wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano kwenda jela kwa kuiba vitu mbalimbali ukiwemo mfugo aina ya Nguruwe mali ya mwalimu wa shule ya sekondari Kiteto
Hukumu hiyo imetolewa leo Desemba 7, 2022 na wawili hao ambao ni John Solomon (25) na Sadick (33) walishtakiwa kwa makosa manne, likiwemo la kuvunja nyumba, kuiba godoro, shuka, neti na kitanda, pamoja na kuiba mfugo aina ya Nguruwe na kupatikana na vitu vya wizi ikiwemo nyama ya nguruwe ya mwalimu huyo.