Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Mzee Yusuph Makamba akiwa Dodoma leo anaposhiriki Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM ameongea na Waandishi wa Habari ambapo amesema Nchi ni kama nyumba, kama ambavyo Mtu hawezi kumaliza matatizo yote ya nyumbani kwa pamoja ndivyo ambavyo Serikali au Chama haiwezi kumaliza matatizo yote bali inayashughulikia kwa awamu.
Akijibu swali la Mwandishi kuhusu nchi kukabiliwa na maji na umeme amesema;
“Nchi ni kama nyumba huwezi kuwa na vyote huko nyumbani, Nchi ni kama nyumbani wewe nyumbani umeyamaliza yote?, Baba yako ameyamaliza yote?, unaitaka CCM iingie leo imalize ni Chama gani hicho.”
“Ubora wa Chama unapimwa katika sera zake ndizo zinazowapeleka Ikulu, mwaka 2025 tunakwenda Ikulu, Wapinzani wajue 2025 hamna kitu”
Kuhusu Mawaziri kugombea Ujumbe Halmashauri Kuu (NEC) amesema “Waziri ni Mwanachama Uwaziri kesho utaondoka Chama kinahitaji Wataalamu, mmemuacha kwakuwa ni Waziri kesho mna nani? Uwaziri ni koti tu amevaa leo jioni Mama Samia anaweza akauondoa mtamkosa.”