Kufuatia serikali na mashirika mbalimbali kuendelea kupiga vita suala la ukeketaji mkoani Mara, jamii ya Wakurya wilayani Tarime imebuni mbinu mpya za ukeketaji kwa kuwavalisha wasichana nguo za kiume baada ya kufanyiwa Ukeketaji.
Akizungumzia suala hilo Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Michael Mntenjele, amesema atawachukulia hatua kali wale wote watakaojihusisha na suala la ukeketaji kwani taarifa zote zimemfikia na wao wanafanya ufutiliaji wa kuwabaini wale wote wanajihusisha na ukeketaji huo.
Suala la ukeketaji pamoja na tohara ambayo siyo salama vinatajwa kuchangia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi pamoja na uwepo wa ndoa za utotoni na mimba za utotoni kwa watoto waliofanyiwa tohara hiyo.