Wananchi wavamia gari la mafuta lililopata ajali, wakimbizana kuchota!

Baadhi ya Watanzania ni kama hawajifunzi!


Unalikumbuka tukio la takribani watu 71 kufariki dunia mwaka 2019, Msamvu mkoani Morogoro baada ya kuchota mafuta ya petroli kwenye eneo la ajali kisha moto kulipuka?

Basi hilo halikuwa funzo kwa baadhi ya watu, kwani tabia hiyo inaendelea.

Lori lililobeba shehena ya Mafuta ya Petroli limepata ajali na kuanguka katika eneo la segera Wilayani Handeni mkoani Tanga

Baadhi ya wakazi wa Segera walijitokeza na kuanza kuchota mafuta, hata hivyo muda mfupi baadaye polisi wamefika eneo hilo na kuwatawanya wananchi hao na hivyo kuepusha ajali ambayo ingetokea endapo moto ungewaka katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bi. Siriel Mchembe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Handeni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo

"Nalipongeza Jeshi la Polisi Handeni kwa kufanikiwa kudhibiti wananchi waliokuwa wanachota mafuta kwenye Gari la mafuta ya petrol lililopata ajali Segera. Hakika Mungu awabariki, wananchi chondechonde tusirudie tenaaaaaa!" - DC Siriel Mchembe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo