"Wanalipishwa 22,000 za kadi ya Kliniki Kwa nini?" Mbunge ampigia simu DMO Live

Mganga mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Dkt. Ligobert Kalisa amesema atafuatilia madai ya wananchi wa kijiji cha Lugoda kata ya Itundu wilayani hapo kumueleza Mbunge wao Festo Sanga kwamba wanatozwa fedha za kadi za kliniki kwa akina mama tofauti na maelekezo ya serikali kwamba kadi hizo zinatolewa bure

Akiwa kwenye ziara katika kijiji hicho leo Desemba 20,2022 Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga amelazimika kumpigia simu Mganga mkuu wa wilaya na kumpa malalamiko hayo ya wananchi ambapo mganga mkuu amesema hana taarifa ya malalamiko hayo ya wananchi hivyo amepokea na atafuatilia kwa hatua zaidi haraka iwezekanavyo

Mbunge Sanga amesema "Wakienda kliniki tu wakiandikisha kadi mama mjamzito ni shilingi 22,000/= na kadi imeandikwa haiuzwi, kwa nini analipia shilingi 22,000/=, ripoti niliyonayo kwenye mkutano hapa na ninaomba DMO hili ulifanyie kazi haraka sana, nipo na kina mama hapa kujifungua wanalipa shilingi 50,000 wakiona sura yako nzuri nzuri, wakiona kama huna hela unalipa 25,000/- na 30,000/-"

Akijibu madai hayo Mganga Mkuu Dkt Kalisa amesema hayo malalamiko yaliyosemwa na wananachi hao kupitia Mbunge hayaruhusiwi kwa kuwa kadi hizo zinatolewa bure na hakuna kulipia gharama za kujifungua kwa mama Mjamzito wilaya ya Makete hivyo madai hayo ameyapokea na atayafanyia kazi mara moja

"Haiwezekani, Nimelipokea Mheshimiwa nitalifanyia kazi kesho" amesema Mganga mkuu wakati akijibu simu aliyopigiwa na Mbunge.

ANGALIA VIDEO HII HAPA UONE ALICHOKIFANYA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo