Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar limesema linawashililia watu watatu kwa tuhuma za makosa ya kuteka nyara na kulawiti mtoto mwenye umri wa miaka 12 huku mmoja kati ya wahusika wa tukio hilo akidaiwa kutoroshwa alipokuwa Gerezani kwa tuhuma za ulawiti
Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Zanzibar ACP Zubeir Chembera wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Visiwani Zanzibar
ACP Chmebera amesema tukio hilo limetokea Disemba 12, 2022 majira ya saa 1 asubuhi huko Chukwani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja ambalo limewahusisha watu watatu akiwemo mganga wa kienyeji ambae mtoto huyo alihifadhiwa kwake kwaajili ya kufanyiwa dawa ili kumfanya mtuhumiwa aliyetoroshwa Gerezeni kutoonekana.