Wanafunzi 10 wa kike shule ya msingi Lembapuli kata ya Loolela Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wametolewa mahari katika maandalizi ya kwenda kwa waume zao wakati wakisubiri matokeo ya mtihani wa darasa la saba
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Musa Mgeta amesema kuwa jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani mwaka huu ni 26 kati yao 21 wamefaulu na watano wamefeli ambapo wanafunzi 10 wa kike ambao walitolewa mahari wamefaulu.
Shule hii ilianzishwa mwaka 2003 huwa na kawaida ya kufaulisha wanafunzi wawili mpaka wanne hivyo jamii ya kifugaji ilipo shule hiyo ilizoea kutoa mahari kabla ya matokeo kutoka ambapo Mkuu huyo wa shule ametoa onyo kwa watakao oa wanafunzi hao kuwa sheria kali dhidi yao zitachukuliwa.