Sheria mpya! Ukichepuka, jela mwaka mmoja

Bunge la Indonesia linatarajiwa kupitisha baadhi ya marekebisho ya sheria mpya za makosa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kufanya ngono nje ya ndoa.


Marekebisho hayo ya sheria yatahusisha pia kosa la kuishi na Mume au Mke bila kufunga ndoa, kumtusi Rais au Taasisi za Serikali pamoja na kutoa maoni yoyote yanayokinzana na itikadi ya Serikali ya Indonesia.

Naibu Waziri wa Sheria nchini Indonesia, Edward Omar Sharif Hiariej amethibitisha kufanyika kwa marekenisho hayo ya sheria katika kuboresha kanuni na adhabu dhidi ya makasa ya kihalifu yanayopishana na maadili ya nchi hiyo ambapo mpaka kufikia tarehe 15 desemba mwaka huu, Bunge la chini hiyo litapitisha miswada mbalimbali ya sheria hizo.

Baadhi ya mabadiliko ambayo yatafanywa ni pamoja na kifungu cha sheria kinachoweza kuruhusu adhabu ya kifo kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha na kuharamishwa kwa utoaji mimba, isipokuwa waathiriwa wa ubakaji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo