Serikali ya Kitaifa nchini Kenya itamhifadhi mtoto Junior Sagini ambaye macho yake yalitolewa pamoja na dada yake ili wakaishi katika nyumba mpya ambayo ni salama.
Waziri wa Utumishi wa Umma na Jinsia Aisha Jumwa alisema wawili hao sasa watatunzwa na serikali.
Gavana wa Kisii Simba Arati alisema Jumwa alimpigia simu Jumatatu kuamuru wawili hao wahamishwe hadi katika nyumba mpya ya usalama jijini Nairobi.
"Nina furaha CS amejitolea kutusaidia kuhusu suluhisho la nyumba salama. Watoto watakuwa salama zaidi huko," Arati alisema.
Alisema inashukiwa kuwa dadake Sagini alinajisiwa mara kwa mara na hivyo kuhitaji kuhamishwa hadi mahali salama.
Mama wa watoto hao wawili pia alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa utelekezaji wa watoto.
Sagini, 3, alishambuliwa na kung'olewa macho Alhamisi usiku huko Ikuruma huko Marani Kisii.
Mshukiwa mmoja amefikishwa mahakamani kwa kosa la kujaribu kuua.