Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema fedha zinazotumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa maarufu kama Standard Gauge Railway (SGR) zinatokana na mkopo wa nje na si fedha za ndani.
Rais Samia amesema hayo leo Jumanne, Desemba 20, 2022 wwkati Alakizungumza katika Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa SGR (Tabora - Kigoma), amesema wamekopa Dola Bilioni 10.04 (Takriban Tsh. Trilioni 23.3) ili kukamilisha mradi huo
Amesema, "Wale wanaosema awamu hii imekopa sana, ndiyo awamu ambayo imejenga reli yote. Pia, tusingeweza kujenga kwa pesa za ndani. Tunakopa ili tujenge kwa maendeo endelevu ya leo na baadaye, kila tunapohisi kuna faida tutaendelea kukopa"
Ameongeza "Niwaambie Wizara ya Fedha hizo taarifa za mikopo zinatoka kwenu, lakini unapokopa ni uungwana kulipa. Sisi hatujawa wa kuomba msamaha, lazima tulipe.."