Polisi Mwanza watangaza msako wa fisi

Baada ya kutokea tukio la mtoto Emanuel Marco Nyangela kufariki dunia kwa kuliwa na fisi katika Kijiji cha Mwangika kata Mwabomba wilayani Kwimba mkoani Mwanza, kamanda wa polisi mkoa huo Wilbroad Mutafungwa amefika katika Kijiji hicho na kuahidi kushirikiana na vyombo vingine vya serikali


Pamoja na wakazi wa Kijiji hicho kuwasaka usiku na mchana fisi hao ili wasiendelee kuleta madhara kwa binadamu


Kamanda Mutafungwa baada ya kufika katika Kijiji hicho amezungumza na dada wa Emanuel aliyejaribu kupambana na fisi ili kumnusuru mdogo wake huyo


‘Walipofika pale mbele yake ndani ya shamba yule fisi alimkamata Ema na kumrusha mbali na kumbeba na kumuweka mbele na kuanza kumvuta Ema mkono na mkono wa Ema ukakatika’


Tukio la mtoto Emanuel kuliwa na fisi lilitokea juzi majira ya jioni na kuwaacha njiapanda wakazi wa Kijiji hicho, ambapo diwani wa kata hiyo ya Mwabomba Amede Sostenes na mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Mwangika Germanus Masala wamesema mbali na wakala wa misitu TFS na jeshi la polisi lakini kuna watalaamu wa kudhibiti fisi wataungana nao kwenye msako huo


‘Na sisi sasa wale tumemaliza kuongea nao muda wowote kuanzia sasa wanaweza kuja hapa wapo zaidi ya mia na mbwa wa kutosha wale ndio wataalamu lakini pia tutashirikiana na hawa wa maliasili tutaunga nao kuhakikisha hili zoezi tunalifanikisha tunawakamata na kuwauwa fisi wote hata kama wamejificha ndani ya nyumba’


‘Tulipojaribu kukagua tukagundua fisi hakuwa mmoja walikuwa wengi ila huyu binti alijitahidi kumkinga mdogo wake kwaweli Mungu amesaidia’


Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ametoa maelekezo kwa viongozi  wa serikali za mitaa na kata mkoani humo kukaa na wananchi kujua kama wanaishi kwa hofu na kutoa taarifa katika vyombo husika ili hatua zichukuliwe huku afisa wa mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori TAWA wilaya ya Kwimba Kurwa Adrian akiahidi kushiriki kikamilifu katika msako wa kuwatafuta na kuwaangamiza fisi hao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo