"Mimi ni katika wale wanaopiga debe wazi kabisa bila aibu, kwamba mama anastahili kuongezewa muda, akimaliza 2025 tumchague tena hadi 2030, tuna hakika akifika huko atakuwa ametufanyia kazi nzuri kwa mujibu wa katiba yetu atakuwa ndio wakati wa kupumzika"
"Rais akifika 2030 atakuwa ameacha alama nzuri sana kwenye demokrasia ya nchi yetu, ndio maana unaona vyama vya siasa wanapumua, nchi inapumua, ameifungua nchi, yupo tayari kwa maridhano, uhuru wa kujieleza mkubwa, tukimpa muda huu wa kutosha wa kikatiba atafungua nchi vizuri"
"Rais Samia amerudisha matumaini mahali ambapo watu walianza kukata tamaa, amerudisha furaha mahali ambapo watu walianza kuvunjika moyo, amerudisha upendo mahali ambapo kulikuwa na chuki pengine, na ametuleta pamoja kama watanzania, jambo hili ni kubwa sana"