Timu ya Simba Sports Club imerejea kileleni mwa ligi kuu ya NBC kwa alama 34 baada ya kuitandika bila huruma timu ya Coastal Union ya jijini Tanga kwa mabao 3 - 0 mtanange uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Desemba 3,2022
Mabao yote ya Simba yamepatikana kipindi cha pili ambapo yamewekwa kimiani na Moses Phiri (magoli mawili na Clatous Chama goli 1
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Makocha wa timu zote mbili wamezungumzia mchezo huo huku Juma Mgunda akijinadi kwamba yeye ni mwajiriwa wa Simba hivyo kusingekuwa na mserereko licha ya kwamba aliwahi kuwa kocha mkuu wa Coastal Union