Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dkt. Hamis Kigwangala amempa onyo kali KIGOGO ambaye wamekuwa wakijibizana mitandaoni hasa katika mtandao wa twitter kuwa hamuogopi na yuko tayari kupambana naye
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete unapofanyika mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kigwangala amesema yeye ni Chifu, na asili ya machifu ni kupmbana na sio kukimbia vita
"Sina chembe ya uoga hata kidogo kwenye damu yangu kwa sababu ni Chifu, umeelewa, Wakati muafaka ukifika nitapigana yaani kama kuna mtu mmoja unamjua jasiri kamtafute mlinganishe na mimi pengine huyo ni mfano tu, niko makini kivita kwa hiyo nachagua silaha, ukiwa makini kivita haupigani ovyo ovyo, na ndio maana jana nimemjibu huyu muheshimiwa hapa jana nimeamua ku-withdraw(kuondoa), kwenye vita kuna mkakati wa kwenda mbele na kuna mkakati wa kurudi nyuma, na kurudi nyuma hata siku moja isitafsiriwe ni kwamba umeshindwa" amesema Kigwangala