Mwingine adakwa kwa kuiba mtoto wa wiki 3 Songwe

Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Plaxeda Msanganzila (28) kwa tuhuma za kuiba mtoto wa wiki tatu.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo akiwa na lengo la kumfurahisha mpenzi wake baada ya kutafuta mtoto kwa miaka 9 bila mafanikio.

Tukio hilo limetokea Disemba 12 mwaka huu katika Mji wa Mlowo, ambapo mtuhumiwa huyo alimchukua mtoto kwa mama yake na kuondoka naye, akidai kuwa anakwenda kununua maandazi, huku akimuacha mama wa mtoto katika kibanda cha chips.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo