Mwanafamilia anayeshukiwa kumng'oa macho mtoto kuendelea kushikiliwa


Mshukiwa mmoja amefikishwa mbele ya mahakama kuhusu kisa cha Alhamisi usiku ambapo mtoto wa miaka 3, Junior Sagini kutoka Marani, Kitutu Chache Kaskazini alipatikana akiwa ameng'olewa macho na watu wasiojulikana.


Hata hivyo, mahakama imeruhusu Alex Ochogo, 26, kuzuiliwa kwa siku tano zaidi katika Polisi wa Rioma huku wapelelezi wakiendelea na uchunguzi zaidi.

Washukiwa wengine zaidi, akiwemo mwanamke mmoja, bado wanasemekana kutoweka huku madaktari katika Hospitali ya Macho ya Kisii wakimruhusu Sagini kuenda nyumbani siku ya Jumapili.

Ogogo alichukuliwa mnamo tarehe 14 mwezi huu na kuzuiliwa katika polisi wa Rioma. Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Christine Ongweno kwa madai ya kujaribu kuua.

Mahakamani, upande wa mashtaka ulisema, mshukiwa alionekana mara ya mwisho akiwa na mtoto huyo kabla ya kugunduliwa akiwa ametobolewa macho.

Mwendesha mashtaka Hillary Kaino aliomba muda zaidi wa kufanya uchunguzi zaidi kuhusu shambulio hilo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 23 Disemba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo