Mchungaji anayezingirwa na utata James Ng’ang’a amewashauri washirika wa Kanisa lake la Neno Evangelism kuwaombea mipango ya kando ya waume zao wapate kujaliwa bwana zao.
Akihubiri katika ibada kanisani mwake hivi karibuni, Ng’ang’a aliwaambia wanawake walioolewa kuacha kuomba mabaya kuwapata hawara za waume zao, bali wanapaswa wawaombee nao pia waolewe.
"Nasikia mnasema mpango wa kando akufe. Wamama wanapenda hiyo sana. Sema bwana Yesu bariki mpango wa kando mpatie bwana yake," alisema pasta huyo.
Zaidi ya hayo, Ng'ang'a aliwatetea mpango wa kando akisema, hawapaswi kulaumiwa kwani mara nyingi ni wanaume ndiyo huwavizia.
"Bwana yako ndiye mpango wa kando, ndiye anatanga tanga tanga. Basi kwanza ua bwana yako... Na umesema Yesu asifiwe, hatujaitwa kuua," aliongeza.
Chanzo:Tuko