Mhubiri Elisha Muliri amechemsha mtandao baada ya kutoa ushauri mzito kwa kina dada ambao wana wachumba.
Mhubiri huyo alisema kina dada wanafaa kuwaenzi wachumba wao kiasi cha kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii.
Muliri anashangaa itakuwa vipi kipusa kumficha ndume ambaye amekuwa akilipa bili za nyumba ikiwamo kugharamia mavazi. "Mwanamke umeolewa, unajiweka kwenye profile ya WhatsApp ama ya Facebook, na kulegeza macho. Kwa nini unaweka picha yako? Si umeshaolewa? Weka picha ya mume wako," alisema Muliri.
Anasema kama umeolewa mambo yako na soko yamekwisha na sasa unafaa tu kumshabikia mume wako. Huyo mwanaume ambaye humuweki kwenye profile ndiye anakulipia nyumba, anakununulia chakula, anakulishia watoto," aliongeza mtumishi wa Bwana. Ni uashauri ambao umewasha moto mkubwa mtandaoni kina dada wakipinga vikali kuhusu wanachofaa kufanya.
Hata hivyo, ndume wengi wamekubaliana na mtumishi huyo wa Bwana waksiema wanafaa kupigiwa debe pakubwa kutokana na juhudi zao kwa wapenzi wao.
Chanzo: TUKO.co.ke