Stori ya kushangaza iliyotufikia ni juu ya tuhuma za mama kuwavuta sehemu za siri watoto 3 wa kiume huko Kimbuni Pemba, imeonekana kugusa hisia za watu wengi huku mama huyo anayetuhumiwa akikana kufanya hivyo na kudai yupo tayari kuwajibika ikiwemo kula yamini
Habari hii imesogozwa na Hassan Msellem, mwakilishi wa Clouds FM Radio huko Pemba Zanzibar, ambapo katika mahojiano MamamMzazi wa watoto hao amekiri kuwa wamefanyiwa hivyo na mama wa kufikia, huku mama huyo pamoja na baba mzazi wa watoto hao akisema ni uongo na hayupo tayari kumsamehe mama wa watoto hao wala watoto wenyewe kwa uongo huo waliomzushia mama yao wa kufikia ambaye ni mke wake wa sasa.
Tazama video