Wanafunzi 1, 073, 941 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022 wakiwemo wavulana 514, 846 na wasichana 559, 095 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Desemba 14, 2022 na Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2023 imeongezeka kwa wanafunzi 166, 139 sawa na ongezeko la asilimia 18.30 ikilinganishwa na wanafunzi 907, 802 walopata alama ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.
BONYEZA <<<<HAPA>>>> KUONA MAJINA HAYO