Mwanaume anayedaiwa kuwa ni mchungaji wa kanisa ambalo halijafahamika mara moja aliyetambuliwa kwa jina la Abdiel Raphael mkazi wa Mtaa wa Uwanja mjini Geita anadaiwa kufariki siku ya nane baada ya kufunga kwa maombi aliyopanga kuyafanya kwa muda wa siku 30 mfululizo.
Imeelezwa kuwa baada ya kufariki Disemba 2 mwaka huu ndugu wa mtumishi huyo waliuhifadhi mwili wa marehemu ndani kwa lengo la kuufanyia maombi ya kumfufua wakiamini kuwa atafufuka jambo ambalo halikufanikiwa.
Baada ya siku 6, majirani walishtushwa na harufu mbaya ikitoka ndani ya nyumba ya mchungaji huyo na kubaini uwepo wa mwili wa marehemu.