Jeshi la Polisi limemkamata, Joseph Mzava (19) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao
Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es Salam ACP Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika oparesheni iliyofanywa na Jeshi la polisi Dar es salaam
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limemkamata Li Naiyong (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha Shilingi Milioni 221.
Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es Salam ACP Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa visivyo rasmi kuwaunganisha watu kwa simu kufanya mawasiliano nje ya nchi kinyume na sheria za mamlaka ya mawasiliano Tanzania.