Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Sabasaba, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara, Amina Ally, (16), anadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kushindwa kujibu swali darasani, na kupelekea kudondoka na kupoteza fahamu akiwa shuleni hapo.
Marehemu anadaiwa kufanyiwa kitendo hicho Oktoba 20 mwaka huu, na mwalimu aliyafahamika kwa jina la Masumbuko, na kwamba amefariki dunia jana Desemba 20, 2022, wakati alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.
Juma Hassan ni ndugu wa marehemu ambapo pamoja na mambo mengine akaeleza uchugunzi uliofanywa na madaktari ambapo umebaini kwamba mishipa ya pua ilikuwa imekatika hali iliyopelekea kuvuja damu muda wote, huku akitoa ombi kwa serikali.