Kijana Amtunuku Nyumba Maridadi Mama Yake Mzazi

Akiwa amelelewa kijijini Busia, Joseph Ombeva alikuwa na ndoto ya kumjengea mama yake mpendwa nyumba nzuri kwa sababu ya jinsi alivyojitahidi kumlea yeye na ndugu zake wengine sita.


Sasa, Ombeva anasubiri sana kwa hamu kumuona mamake hatimaye anahamia katika nyumba mpya anayomjengea.


"Babangu alifariki dunia nikiwa mdogo sana na mamangu alitatizika kunilea pamoja na ndugu wengine 6," Ombeva aliambia TUKO.co.ke kwenye mahojiano. “Amenisomesha kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu, nyumba aliyokuwa akiishi nikiwa shule ya msingi ni ile ile aliyokuwa akiishi wakati namalizia masomo yangu ya chuo kikuu, sasa nimeajiriwa hivyo nikasema lazima afurahie matunda ya dhabihu yake ili kuboresha maisha yangu," aliongeza.


Bajeti ya Ombeva ilikuwa KSh 900, 000 kwa nyumba ya vyumba viwili ambayo pia ina sebule, jikoni na stoo. Kufikia sasa, ametumia KSh 720, 000. "Amefurahi sana na anatarajia kuhamia ndani ya nyumba yake mpya mara tu itakapokamilika. Kilichobaki ni kupiga plasta ndani na nje, kisha kupaka rangi," alisema. Mnamo Novemba, mwanamume Mkenya anayeishi Marekani alirudi na kukamilisha nyumba ambayo ilikuwa imeachwa na marehemu babake miaka mingi iliyopita.


Ryan alikuwa na umri wa miaka kumi tu wakati wa kifo cha baba yake, lakini anakumbuka wazi kwamba familia yao iliteseka sana kwa kutokana na baba yao kuwaacha. Mbali na kukamilisha nyumba hiyo, pia aliandika ujumbe mzito kwa baba yake mpendwa, ambaye aliaga dunia miaka 30 iliyopita katika ajali ya kuogofya ya barabarani.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo