Mtu mmoja anayefahamika kwa jina moja la Abdallah anatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kumuua mkewe, Pili Mang’ota (38) mkulima na muuza mbogamboga mkazi wa Sanze, Kata ya Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Pius Lutumo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ameeleza kuwa Abdallah alifanya mauaji hayo baada ya kuambiwa kuwa mtoto wanayemlea si wa kwake.
Kamanda Lutumo amesema tukio hilo lilifanyika mnamo Desemba 17 mwaka huu saa nane mchana ambapo marehemu aliaga nyumbani kuwa anaenda kuchuma mboga shambani na hakurudi tena hadi mwili wake ulipokutwa kichakani ukiwa umefukiwa na kuharibika.