Ajali ilivyoua watu watano Mkoani Morogoro

Watu watano waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro wametambuliwa wakiwemo mume na mke, ambao pia ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa Desemba 26,2022, eneo la Iyovi, Kata na Mikumi, wilayani Kilosa, ikihusisha gari ndogo aina ya Toyota Allion yenye namba IT 6954 DNN, iliyogongana uso kwa uso na kwa uso na gari kubwa la mafuta aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili RAE 518C yenye tela namba RL 2686.

Amesema gari ndogo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma, ilikuwa ikiendeshwa na Festo Eliuzima Shoo na gari kubwa lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Morogoro lilikuwa likiendeshwa na Muthoni Richard raia wa Rwanda.

Musilimu alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo, kutaka kuyapita magari mengine bila tahadhari, ndipo wakakutana uso kwa uso, ambapo dereva huyo wa gari ndogo ni miongoni mwa waliofariki.

Wengine ni Grayson Ng’obo mkazi wa Mbeya na Janeth John Luvanda (40), ambao kwa mujibu wa Kamanda huyo taarifa walizopata Grayson na Janeth ni mume na mke.

Marehemu Grayson Ng’obo na mkewe Janeth John Luvanda enzi za uhai wao. Aliwataja wengine waliofariki dunia ni Oswald John Luvanda (42) mkulima na mkazi wa Mbeya, ambaye ni ndugu wa Janeth Luvanda na John Davis Haule (37) Mwalimu wa shule ya Wanging’ombe iliyopo mkoani Mbeya.

Katika hatua nyingine uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kanda ya ya Mbeya umetoaa taarifa kuwa Grayson Ngogo na Janeth Luvanda waliofariki kwenye ajali hiyo ni wanafunzi wa chuo chao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wanafunzi hao walifariki kwenye ajali iliyotokea mkoani Morogoro na kuwa taratibu nyingine zitaendelea kutolewa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo