Watoto tisa wa familia moja waungua Moto, mmoja afariki

Mtoto amefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa baada ya nyumba walimokuwa wamelala kushika moto katika mtaa wa Buhare Mjini Musoma.


Moto huo ulizuka usiku wa kuamkia Novemba 5, 2022 na kuunguza watoto hao tisa wa familia moja ambapo mmoja alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.


Watoto watatu kati ya wanane hali zao ni mbaya ambapo wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.


Akizungumzia tukio hilo leo Jumatatu Novemba 7, 2022, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana huku mzazi akidai chanzo ni moto wa mshumaa.


"Ni kweli tukio limetokea, mtoto mmoja amefariki na wengine watatu hali zao ni mbaya, tayari tumeanza uchunguzi tutatoa taarifa kamili baada ya kukamilisha uchunguzi wetu " amesema Magere kwa njia ya simu.


Baba mzazi wa watoto hao, Emmanuel Magiri amesema kuwa tukio hilo lililotokea baada ya umeme kukatika ndipo watoto hao waliokuwa wamelala pamoja kwenye chumba kimoja kuamua kuwasha mshumaa kwaajili ya kupata mwanga.


"Baada ya kuwasha mshumaa walipitiwa na usinguzi ndipo godoro walilokuwa wamelalia likashika moto na kusambaa chumba kizima" amesema.


Zaidi bofya<<HAPA>>>>

Via Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo