Video ya Bi Harusi Akisafirishwa Kwenye Paa la daladala Yasisimua

 

Video ya bibi harusi aliyeketishwa kwenye paa la daladala imewashangaza watu wengi katika mitandao ya kijamii.

Video hiyo ambayo ilinasa tukio hilo lisilo la kawaida ilichapishwa kwenye TikTok na Mmesidibe.


Katika kipande hicho kifupi, bi harusi alikuwa peke yake kwani bwana harusi hakuwepo, lakini watu wengi walimzunguka. Ilionekana kana kwamba basi hilo lilikuwa limepangwa kwa ajili ya kumbeba pekee, lakini jambo la kushangaza ni kwamba alikuwa juu ya paa la gari hilo.


Bibi harusi alionekana kutoshangaa wala kupinga wakati ulipofika wa yeye kupanda basi, na kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa huenda huo ni utamaduni wao. Hili halijathibitishwa hata hivyo. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo