Video Mpya : RICHIEO - NEW LEVEL


Richie Obiri maarufu kama RichieO ameachia kazi yake mpya iitwayo NEW LEVEL ikiwa katika miondoko ya amapiano.
RichieO ni Msanii mwenye Asili ya Nigeria aliyezaliwa nchini Marekani na kukulia nchini Uingereza wakati wa miaka yake ya mapema.

Baadaye alikwenda kuishi nchini Ghana (Afrika Magharibi) kabla ya kurejea Marekani na kufanya makazi ya kudumu. 

RichieO alianza kuimba katika kwaya ya kanisa la mtaani na baadae akachaguliwa kuwa kiongozi wa Praise katika sehemu yake ya ibada huko Marekani. 

Katika maisha yake yote muziki umekuwa na jukumu muhimu katika maisha yake huku akina Fela Kuti, Sade, Craig David na WizKid wakiwa na ushawishi mkubwa katika sanaa yake Ingawa jumbe za Injili/Inspirational ni maudhui ya nyimbo zake, Afrobeats ndiyo aina anayojieleza vyema zaidi na hivyo Mashabiki wanahaidiwa kazi kubwa toka kwake.

Kwa kuwa karibu na Richieo unaweza kumfuatilia kupitia Twitter @Richieomusik



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo