Kigwangalla awalipua Dkt. Bashiru na Jaji Warioba

Mbunge wa Nzega Vijijini na aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameibuka na kudai kuwa dhambi aliyoifanya Mbunge wa kuteuliwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt Bashiru Ally kwa kudharau, kukejeli, Kunajisi na kudogosha juhudi za Rais kwenye kuboresha maslahi ya wakulima haistahili huruma.


Chapisho la kwanza la Dkt. Kigwangalla wakati Dkt Bashiru anateuliwa kuwa Mbunge na kuondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Kigwangalla ametoa maneno hayo kupitia chapisho lake aliloandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ikiwa ni sehemu ya kuonesha kutomuunga mkono Dkt Bashiru kuhusu kauli yake juu ya juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.

Ikumbukwe awali wakati Dkt Bashiru anateuliwa kuwa Mbunge na kuachia wadhifa wake wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tukio hilo lilipokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wadau wa siasa na wananchi baadhi wakimcheka na kumkejeli lakini kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter Dkt Kigwangalla aliandika na kumkingia kifua Dkt Bashiru akiamini hatua ile ilikuwa ni riziki mpya na mipango ya Mungu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo