Angalia ajali ya Basi na Lori ilivyoua watu huko Dodoma

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi la Arusha Express kugongana uso kwa uso na lori.


Ajali hiyo imetokea leo Jumapili Novemba 13, 2022 mchana eneo la Veyula Kata ya Makutupora mkoani Dodoma.

Angalia Video ya ajali hiyo hapa chini:-

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibiti ajali hiyo na kusema bado wanafuatilia chanzo cha ajali na athari zaidi zilizotokana na ajali hiyo.


"Ni kweli ajali hiyo ipo, watu watano wamepoteza maisha katika eneo la ajali na wengine kujeruhiwa na wamekinbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu," amesema Otieno.


Hata hivyo amesema taarifa kamili zitatolewa baadaye kwani Polisi walikuwa eneo la tukio kufuatilia.

Basi hilo lilikuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya limegongana uso kwa uso na lori la kampuni ya ujenzi ya China Hydropower.


Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo