Aliyekanwa na Simba afikishwa mahakamani

ALIYEKUWA kocha wa makipa wa Klabu ya Simba Muharami Sultan (40) na wenzake 6 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya.


Mashitaka hayo yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace  Mwanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Merry Mrio na Wakili wa utetezi Daudi Mzeri.


Wengine ni pamoja na Mmiliki wa Kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi seif, Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu maarufu mbonde (54) mkazi wa kisemvule na John John maarufu Chipanda (40) ambaye jukumu lake kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy na Sara Joseph.

Mwanga ameieleza mahakama kuwa watuhumiwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya usafilishaji wa madawa ya kulevya


Katika hati ya mashitaka imeeleza kuwa mnamo tarehe 27,2022  Ilala Dar es Salaam walikutwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina heroin yenye uzito wa kiliglamu 27.1.


Pia shitaka la pili wanatuhumiwa kulitenda mnamo tarehe 4,11 2022 ndani ya Wilaya ya  Mkuranga Pwani walikutwa wakisafirisha madawa aina heroin yenye uzito wa kiliglamu 7.79.


Baada ya kusomewa mashitaka hayo Hakimu Mrio amewaeleza watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwani Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikilizwa kesi hiyo.

Wakili Mwanga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaemdelea.


Kesi hiyo imehairishwa hadi Desemba 5,2022 kwa ajili ya kutajwa na watuhumiwa wamerudishwa rumande.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo