Albino auawa, anyofolewa Mkono wake wa Kulia

MKAZI wa Ngula mkoani Mwanza, Joseph Msongoma (49) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) ameuawa kwa kukatwa panga na watu wasiojulikana na kisha kutokomea na mkono wake wa kulia.


Inasemekana tukio hilo limetokea Novemba 2, 2022 majira ya saa nne usiku baada ya watu hao kufika nyumbani kwa Joseph na kumwita jina lake kisha kumkata mkono wake wa kulia na kutokomea nao kusikojulikana.


Akizungumza na chombo kimoja cha habari kupitia simu, Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (Shivyawata) Mkoa wa Mwanza,  Alfred Kapole, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vitendo hivyo na kuiomba serikali kuwatafuta watu waliotekeleza unyama huo.


Kapole amesema tukio hilo linalohusishwa na imani za ushirikina linatakiwa kukemewa na serikali kuwachukulia hatua kali watu hao ambao wamekuwa wakitishia usalama wa watu wenye ualbino.


“Hivi kama kweli viungo vya mtu mwenye ualbino vingekuwa vinaleta mali, ingewezekana watu wenye ulemavu huu wakawa maskini?” amehoji Mwenyekiti huyo.


“Zaidi ni watu ambao tunatakiwa kuonewa huruma kwa sababu pamoja na kuwa na ulemavu tunahitaji msaada kwani tuko hatarini kukumbwa na ulemavu wa macho na saratani ya ngozi," amesema Kapole.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo