Wafugaji wanaomiliki Silaha haramu wakumbushwa kuzisalimisha

Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi 


Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo nchini ACP SIMON PASUA amewataka wafugaji wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu kuzisalimisha Jeshi la Polisi na maeneo yaliyoainishwa ili wawekewe utaratibu mzuri wa kuzimiliki kihalali ambapo amesema kuwa Muda wa msamaha umebaki mchache hivyo amewataka wajitokeze kusalimisha silaha ambazo wanamiliki kinyume na utaratibu.


Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini Kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema zaidi ya mifugo elfu kumi mia saba thelathini na nane wamewasili katika kijiji hicho ikiwa ni awamu ya kumi na mbili.


ACP PASUA amesema Jeshi hilo linaendelea kuwahakikishia wananchi wanaohamia katika Kijiji cha Msomera kuwa Mifugo yao iko salama ambapo amewataka kufuata matumizi bora ya ardhi ili kuepusha Migogoro ya wakulima na wafugaji.


Kamanda Pasua amebainisha kuwa zoezi la kuhamisha mifugo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro linaendelea kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo