Wafugaji Waliohamia Msomera waunga mkono Juhudi za uhifadhi



Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi


Wafugaji wa Jamii ya kimasai waliohamia katika kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga wamesema wameamua kwa hiari yao wenyewe kuhamia Msomera kuunga Juhudi za uhifadhi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.


Wafugaji hao ambao wamehamia eneo hilo wakitoka katika mamlaka ya hifadhi Ngorongoro wamesema watalitumia eneo hilo kwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo tofauti na mwanzo walipokuwa katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambapo fursa hiyo hawakuipata.


Hayo wamesema jana Oktoba 09,2022 katika kijiji cha Msomera ambapo baadhi ya wafugaji Wa Jamii ya kimasai mara baada ya kuwasili kwa kundi la kumi na mbili katika Kijiji cha Msomera Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, wafugaji hao wamesema wanamuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jitihada zake za kukuza uhifadhi na utalii alizoanza kuzionesha katika Nchi yetu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo