Mtumizi mmoja wa Facebook amewachekesha wanamitandao baada ya kuachia maoni ya utani mno kuhusu timu ya walemavu ya mpira wa miguu Tanzania kufuzu robo fainali ya kombe la dunia.
Shirika la habari la BBC Swahili kupitia ukurasa wao wa Facebook waliripoti taarifa hizo kwamba timu ya taifa ya mpira wa miguu kwa walemavu, Tembo Worriors, ambayo ni ya kandanda ya wanaume imefuzu robo fainali ya kombe la dunia.
“Timu ya taifa ya walemavu ya Tanzania imetinga robo fainali ya kombe la dunia kwa watu wenye ulemavu baada ya kuichapa Japan 3-1 katika mchezo wa hatua ya 16 bora huko Uturuki. Tanzania sasa itakutana na Haiti waliomfunga Marekani 6-2, katika mchezo wa robo fainali utakaopigwa kesho,” BBC waliripoti.
Baada ya taarifa hizi za kufurahisha, haswa ikizingatiwa kuwa Tembo Worriors ndio wawakilishi wa pekee kutoka bara zima la Afrika, wanamitandao walifurika kutolea maoni yao wengine wakiwapongeza ila kuna mmoja aliyezua utani kupitiliza na kufanya maoni yake kuzungumziwa sana mitandaoni.
Mtumizi huyo wa Facebook kwa jina Jackson Boniface alitoa maoni yake kwa kuwapongeza walemavu hao na kuchagiza zaidi kwamba ni wakati sasa baadhi ya wachezaji wenye viungo vyao vyote kwenye timu ya Taifa Stars kukatwa miguu ili kuongeza nguvu kwenye timu hiyo ya walemavu.