Rais William Ruto Ataka Kila Mkenya Kupanda Miti Mia Moja

Rais wa Kenya William Ruto sasa anataka kila Mkenya kupanda miti ili kupata suluhisho la kudumu kwa tatizo la ukame nchini kupitia utunzaji wa mazingira. 


Akizungumza katika kaunti ya Kirinyaga mnamo Jumamosi, Oktoba 15, Rais alitaka kila Mkenya - watoto wakiwemo - kupanda miti mia moja kila mmoja ili kutatua tatizo la ukame linalohangaisha sehemu kadhaa nchini. 


“Kama uko na mtoto ambaye hawezi kupanda, mpandie miti mia moja. Yule amezaliwa, sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto, apandiwe miti mia moja. Hivyo ndivyo tutahakikisha kuwa kuna mazingira ambayo itatupatia hali, maji, tuweke kwa dam, tumalize njaa," Rais Ruto alisema. 


Ruto alisema kuwa mabadiliko katika hali ya anga yanayoshuhudiwa nchini na barani Afrika kwa jumla ni kutokana na kuharibiwa kwa mazingira. 


Kwa mujibu wa Ruto ambaye alizungumza wakati wa kuidhinisha bwana la Thake katika kaunti ya Kirinyaga, tatizo la sasa la mabadiliko katika hali ya anga linaweza kurekebishwa kwa kupanda miti bilioni tano. “Lazima tufanye wajibu wetu kama taifa; ili tuwe na maji, jinsi ilivyo katika bwawa hili, lazima tuzingatie mazingira yetu kama nchi. Tumefanya uamuzi wa kisera kwamba lazima tupande miti bilioni tano," Ruto alisema. 


“Kila Mkenya, tukiwa milioni 50, lazima apande miti isiyopungua mia moja. Iwe katika boma lako, shamba lako au sehemu yoyote utakayopata. Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya sisi kubadili hali ya anga ili tuweze kuwa na maji, kukuza mimea, kujenga mabwawa, kusindika mazao ya kilimo na kuhakikisha tunastawi.” 

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo