Shule ya Sekondari yakumbana na suala nzito la mimba za mapema

Shule moja ya upili ya katika kaunti ya Lamu nchini Kenya inakumbana na hali ngumu ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanafunzi wajawazito shuleni humo suala ambalo sasa jamii inatafuta suluhu la haraka. 


Shule ya Sekondari ya Hindi ina wanafunzi sita wajawazito huku wengine wakiwa tayari wamejifungua hali ambayo inatia wasiwasi wazazi na viongozi wa jamii "Tunapozungumza, wasichana sita ni wajawazito," Nancy Aira, Naibu Mwenyekiti wa Shule ya Sekondari ya Hindi aliambia Citizen TV. “Nilishiriki ngono kabla ya ndoa kwa sababu ya changamoto za kimaisha kama vile kupata chakula, sabuni ya kufulia sare,” alisema mmoja wa wasichana walioathirika. 


Katika baadhi ya visa, wazazi na walezi hawana habari kuhusu makubwa yaliyowakumba watoto wao kwa sababu wengi wao hujaribu kuficha mimba. "Nilifahamu ujauzito wake tu alipoanza kuzirai; wanavaa mashati makubwa siku hizi. Nilimpigia simu mama yake na kumwambia kuwa msichana wake alikuwa na mimba," alisema Helen Karisa. 


Kando na mimba za mapema, jamii pia ina wasiwasi kuhusu maambukizi ya magonjwa ya zinaa. "Mimba ni ishara za wazi kuwa hawatumii kinga. Baadhi yao ni wajanja sana wanatumia dawa za kupanga uzazi kuzuia mimba lakini vipi kuhusu magonjwa ya zinaa?" "Kama watu hawatatumia kinga kuna hatari ya vijana wetu kuambukizwa kisonono na 'UKIMWI," alisema Hassan Chonda, kiongozi wa jamii hiyo. 


Kwa upande wake, Douglas Katana, alilaumu pombe kwa kuongezeka kwa idadi ya mimba. "Ni starehe ya pombe na starehe ya wanaawake.Watu wamezingatia ulevi, starehe ya kunywa pombe na wanawake ndio hapa imadhiri," alisema. 


Washikadau sasa wanatoa wito kwa wazazi kuwaelekeza watoto wao na kuwaepusha na hali hiyo. Kenya ni nchi ya tatu duniani yenye idadi kubwa ya mimba za mapema. Wizara ya Afya ilirekodi mimba 45,724 za mapema kati ya Januari na Februari mwaka huu ikimaanisha kuwa matineja 724 wanapata mimba kila siku. 

Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo