Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameandika maoni ya kufurahisha baada ya kukutana na yaliyomo kwenye kitabu kilipakiwa mtandaoni.
Katika picha hiyo ya kurasa mbili ambayo ilipakiwa na mtumizi mmoja wa mtandao wa Twitter, inaonesha kitabu cha watoto wa chekechea kinachowatambulisha watoto kwa alfabeti za kuunda maneno kuanzia A mpaka Z, huku kila herufi ikiwa inatambulishwa kwa kitu, mnyama au umbo fulani.
Mtumizi huyo wa Twitter kwa jina Abazz alipakia akisema kuwa mamake alimnunulia dadake mziwanda kitabu hicho ili kujifunza alfabeti.
Lakini maudhui ya kitabu hicho ndio yaliyozua gumzo kali baada ya herufi za alfabeti kuonekana zikiambatanishwa na baadhi ya vitu vya kuzitambulisha kisauti tofauti za majina yao halisi.
Kwa mfano, katika lugha ya kimombo, herufi A inasimamiwa na tunda aina ya tufaha yaani ‘Apple’, lakini katika kitabu hicho, herufi A iliambatanishwa na mti, kwa kimombo ‘Tree’.
Katika kitabu hicho, herufi kadhaa zilionekana kubandikiziwa vitu visivyoendanana herufi hizo hata kidogo, kwa mfano herufi O katika kitabu hicho iliandikwa kwamba inasimamiwa na nyuni, kwa kimombi ‘Bird’
“Mama amenunua kitabu hiki kwa ajili ya dada yangu mdogo 🙆🏽♂️😭.... Nilidhani niko juu 😂🤧 C kwa Farasi & A kwa Mti 😭😫😂” Abazz alilalama kwenye Twitter, jambo ambalo liliwavutia wanamitandao wengi kutolea maoni yao.
“S ni ya Tumbili, R kwa gurudumu, Q kwa mkia, E kwa nyota, P kwa samaki, N kwa theluji, G kwa keki. Wueeh akili yangu inageuka tayari,” mmoja alisema kwa utani.