Mchungaji asimamishwa kazi kwa tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

 

MCHUNGAJI wa Kanisa la Anglikana Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam Edwin Taji, amesimamishwa kutoa huduma ya kichungaji baada ya kudaiwa kumtorosha mke wa muumini wake na kumpangishia nyumba maeneo ya Pugu Kajiungeni.

Madai hayo yametolewa na muumini wa kanisa hilo ambaye ni Mume wa mwanamke huyo Simon Ngalawa mkazi wa Yombo akilalamika kuwa mkewe Ester Makunya kujihusisha kimapenzi na mchungaji Taji.


Ngalawa anadai baada ya kusikia tetesi hizo kutoka kwa waumini na ndugu zake, alibaini kuwa mkewe alianza kuwa na fedha wakati hana kazi wala biashara yoyote, na baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha kwa miaka mitatu ndipo alipoondoka nyumbani na kwenda kuishi Kiwalani ambako inadaiwa alipangishiwa nyumba na kufunguliwa duka na mchungaji huyo.

Je umeshaiona Video hii, hembu iangalie uone

Amesema licha ya kuitisha vikao vya familia, kwenda ustawi wa jamii na Dawati la jinsia lakini ilishindikana mkewe kurudi nyumbani ndipo alipoamua kukutana na viongozi wa juu wa kanisa hilo ili kumshtaki Mchungaji huyo.


Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa Mchungaji Taji amesimamishwa kuhudumu wiki mbili zilizopita huku shauri lake likiendelea kujadiliwa na wakuu wa kanisa hilo.

Chanzo: Nipashe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo