Mwanafunzi achomwa Kisu na Mwanafunzi mwenzie Bukoba

Mwanafunzi Jackson Stephen wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kagemu iliyoko katika manispaa ya Bukoba, amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera, baada ya kujeruhiwa kwa kuchomwa kisu mara mbili katika paja lake la mguu wa kulia, na mtu anayedaiwa kuwa pia ni mwanafunzi, kutokana na kumdai shilingi 4,000.


Akizungumza katika wodi namba moja alikolazwa akiendelea na matibabu, mwanafunzi huyo amesema kuwa alikopeshwa shilingi 3,000 na mwenzake na kumtaka alipe shilingi 4,000 ikiwamo shilingi 1,000 ya riba, fedha ambazo alikuwa hajazipata, na kwamba jana wakiwa katika sherehe ya kuhitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari Bukoba, alimtaka kulipa deni hilo na aliposhindwa kulipa alimchoma kwa kisu.

Kwa upande wake Daktari Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. Emmanuel Sanga, amekiri kumpokea mwanafunzi huyo jana saa kumi za jioni akiwa na majeraha mawili katika paja lake la kulia, akivuja damu nyingi na kumpatia matibabu ya dharura ili kuzuia damu zisiendelee kuvuja.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo