Albert Mbilinyi pamoja na Patrick Malumba ni Wananchi wa kijiji cha
Makangalawe wakizungumza na mwandishi wa habari hii kijijini hapo wamesema mnyama anayedhuru
mifugo yao bado hawajambaini mpaka sasa huku wengine wakihisi kutokana na moto uliounguza miti kijijini hapo huwenda ukawa umewakurupua wanyama wakali waliokuwa wamejificha maporini.
Batweli Chengula ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya Kijiji amesema tukio hilo sio la kwanza kuripotiwa kijijini hapo huku Remijusi Magere ambaye ni Mtendaji wa kijiji hicho akisema alichofanya ni kuujulisha uongozi wa Juu yake kuhusu tukio hilo.
Aldo Mwapinga ambaye ni Afisa mifugo na Uvuvi Halmashauri ya wilaya ya Makete amesema amezipata taarifa hizo na kwa sasa taratibu nyingine zinaendelea baina yao na watu wa pori la akiba la Mpanga Kipengere huku akielezea kuwa tukio kama hilo limejitokeza pia katika kijiji cha Ilungu kata ya Ipepo ambapo taaratibu za kuwapa fidia walioathirika na tukio hilo zinaendelea.
Fredrick Kobelo Ni Kaimu kamanda katika Pori la akiba mpanga Kipengere amesema wamefika maafisa wao katika kijiji hicho na taarifa za awali wamebaini kuwa huwenda mnyama huyo akawa ni Chui licha ya kwamba bado wanaendelea na Uchunguzi zaidi kuhusu mnyama huyo.
Kobelo amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote katika kipindi hiki na kwa yeyote atakayemuona mnyama huyo awasiliane nao.
Habari na Boniface Mwafulilwa