Mume wa mwanamke aliyefariki kisa mchepuko, naye Afariki Dunia

Wiki mbili zilizopita kulikuwa na habari za tanzia kuhusu mwanamke mmoja aliyefariki dunia katika ajali ya barabara alipokuwa akimkimbiza mumewe, Sonnie Bassey baada ya kumfumania na mwanamke mwingine.


Sakata hilo limeibuka tena baada ya taarifa mpya kudai kuwa mwanaume yule naye pia amefariki dunia baada ya kuwa katika hali ya kutojitambua kwa majuma mawili tangu tukio lile kutokea, yeye akiwa kama mhusika mkuu katika kifo cha mkewe.


Kulingana na 9News, hatimaye mwanaume huyo kwa jina Sonnie alishindwa vita dhidi ya mshtuko uliompata na kufariki huku sasa watoto wao wakiwa wameachwa kama mayatima.


“Mke aliyefariki wiki mbili zilizopita alipomwona mumewe akitoka kwenye Shopping Mall ya SPAR akiwa na mwanamke mwingine alipojaribu kuzuia gari la mumewe na Toyota Highlander aliyokuwa akiendesha,” 9News iliripoti.


"Katika harakati za kumkimbia mumewe, alishindwa kulidhibiti gari lililokuwa likienda kwa kasi, na kuacha njia na kuligongesha gari lake kwenye mti, na kuharibu gari hilo kiasi cha kutorekebishwa na pia kujiua papo hapo," habari zaidi zilisimulia.


Iliripotiwa kuwa baada ya kifo cha mkewe, mwanaume huyo alionekana akilia katika kitanda cha hospitali ambapo mwili wa mke wake ulikuwa umelazwa huku akibembeleza maiti hiyo kurudi ili waendelee kulea watoto wao, na pia akijutia tukio zima lililotokea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo