Watu kadhaa ambao wanatuhumiwa kufanya kitendo Cha kinyama kwa kumuua mtoto wa miaka 10 Mtemi Ndambo na kutoweka na ng'ombe aliokuwa nao kondeni katika Kijiji Cha Kakese kata ya Kakese wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, mamlaka ya jeshi la polisi imefanikiwa kuwanasa.
Akiwa katika mkutano wa hadhara Kijiji hapo,Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24,2022 wakati Mtoto huyo akiwa machungani na ndipo alipokutana na watu hao kwa lengo la kuiba Ng'ombe wanne waliokuwa wakichungwa na Mtoto huyo.
Hata hivyo Bi Jamila amesema Ng'ombe hao wamepatikana na wahusika wote wamekamatwa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbugani Boniface Senegali amesema kilio kikubwa cha Wananchi kwa Serikali ni kuwajengea kituo cha Polisi kwani wanadai usalama Kijijini hapo umekuwa mdogo kutokana na wizi kushamiri vikiwemo vitisho.